Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus kucheza fainali ya 21, Coppa Italia

91892ee212.jpeg Juventus watacheza fainali ya 21 ya Coppa Italia ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: eatv.tv

Klabu ya Juventus kutoka Turin nchini Italia imeweka rekodi ya kufuzu fainali ya 21 ya michuano ya Coppa Italia. Baada ya kuifunga Fiorentina kwenye mchezo wa nusu fainali mabao 2-0 na kufuzu kwa ushidi wa jumla wa mabao 3-0 kwenye michezo ya mikondo miwili.

Kwenye mchezo wa nusu fainali ya mkondo wa pili jana usiku Juventus walikuwa wenyeji wa Fiorentina katika dimba la Allianz na waliingia katika mchezo huo wakiwa na faida ya kuongoza bao 1-0. Baada ya kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza. Kwenye ushindi wa mabao 2-0 jana usiku mabao ya juventus yamefungwa na Federico Bernardeschi na Danilo.

Juve Kibibi kizee cha Turin imefuzu kucheza faianli ya 21 ya Coppa Italia ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote na ni mara 5 zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kucheza fainali nyingi ambayo ni AS Roma ambao wamecheza fainali 17.

Juventus ndio mabingwa wa Kihistoria wa michuano hii wametwaa ubingwa mara 14 na katika hatua ya fainali watacheza dhidi ya Inter Milan mchezo utakaochezwa May 11 katika dimba la Olympics Roma.

Chanzo: eatv.tv