Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juventus Kumuongezea Mkataba Matthijs De Ligt

GettyImages 1314009658 1536x1024 Matthijs de Light (kushoto) akiwa na Chiellini

Wed, 17 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Juventus imeingia kwenye mazungumzo na beki wao kati Matthijs de Light wa kuongeza mkataba na miamba hiyo ya Turin hadi mwaka 2025.

De Ligt aliwafanya Juventus walipe kiasi cha €75milioni kama ada ya uhamisho mwaka 2019 wakati wanamsajiri kutoka Ajax, wakati akiwa beki bora kinda duniani kipindi hicho aliposainishwa, lakini ajacheza michezo mingi kama alivyotarajiwa.

Msimu huu amejikuta akiwa anawekwa nje mara kwa mara na wakongwe Leonardo Bonucci and Giorgio Chiellini, mwezi wa oktoba alikiri kuwa hana furaha na nafasi anayopata klabuni hapo, huku akihusishwa na kuhamia kwenye vilabu vya Barcelona na Chelsea.

Japokuwa kuna uvumi huo, lakini Juventus hawana mpango wa kumuachia huku wakizipuuzia taarifa za wakala wake Mino Raiola, De Ligt anamktaba na Juventus ambao unaisha mwaka 2022, huku kukiwa na kipengere cha €150milioni kama ada ya kuvunja mkataba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live