Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juve kama Simba, yafagia kikosi chake

Juve Pc Juve kama Simba, yafagia kikosi chake

Tue, 6 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha la usajili wa wachezaji linaloendelea duniani lina maajabu yake, ambapo timu mbalimbali zinaendelea kusuka vikosi zikiwamo, huku Juventus inayokipiga katika Ligi Kuu Italia (Serie A) ikiwataka mastaa wanane watafute vichaka vipya.

Kama ilivyofanya Simba hapa nchini ambayo imeachana na nyota zaidi ya 10 wazawa na wale wa kigeni, Juventus imeanza kusuka kikosi kipya baada ya kuukosa ubingwa wa Serie A kwa misimu minne ambapo ilibeba Coppa Italia 2020-21.

Hata hivyo, tangu Cristiano Ronaldo alipoondoka katika kikosi hicho kimeishi misimu minne kikijitafuta na kwa sasa hakijajipata licha ya kuundwa na mastaa kibao wa daraja la juu.

Kama ambavyo Wekundu wa Msimbazi walivyopoteza ubingwa wa Ligi Kuu Bara katika misimu mitatu mfululizo ukienda kwa watani zao, Yanga, kule Italia Juventus baada ya kulikosa taji la Serie A kwa miaka minne mfululizo iliyopita,  imeamua kufanya uamuzi mgumu ulioletwa na kocha mpya, Thiago Motta.

Uongozi wa timu hiyo umewaambia wachezaji wanane wa timu ya kwanza ikiwa ni pamoja na straika Federico Chiesa na kipa Wojciech Szczesny waondoke kikosini kwa sababu nafasi zao zinatakiwa kujazwa na vyuma vipya.

Motta anasimamia kusafisha timu kwa ukali, huku akijaribu kuboresha kikosi kilichokuwa na matatizo msimu uliopita ndani na nje ya uwanja, ambacho hakikuambulia chochote kikimaliza katika nafasi ya tatu.

Ingawa Juventus ilitembea msimu mzima ikiwa katika uchunguzi wa upangaji matokeo kutoka kwa mamlaka za uendeshaji wa soka nchini humo, awali ilipokonywa pointi 15 kabla ya kurejeshewa.

Mashabiki wa timu hiyo wanakikumbuka kikosi bora kilichodumu muda mrefu sambamba na upepo mzuri uliowabeba kwa misimu tisa wakibeba Serie A, lakini sasa

wamelikosa taji la Serie A katika misimu minne iliyopita baada ya kushinda kwa misimu tisa mfululizo. Misimu miwili iliyopita walimchukua Massimiliano Allegri na kumuweka kando Motta wakitaraji kuanza naye msimu ujao kama kocha.

Kwa Chiesa, nyota mkongwe katika kikosi hicho ni mmoja wa wachezaji wanane ambao wanatakiwa kuuzwa katika dirisha hili, kama ilivyoripotiwa na Fabrizio Romano. Mchezaji wa zamani wa Arsenal na kipa wa muda mrefu wa Juventus, Szczesny nafasi yake itachukuliwa na kipa mpya huku yeye akijiunga na wachezaji wawili wa zamani wa Ligi Kuu England wanaotarajiwa kuondoka Turin.

Motta alisisitiza mbele ya wanahabari hivi karibuni baada ya mechi ya kirafiki ya maandalizi ya msimu ujao dhidi ya Brest kuwa, “(Wachezaji hao) wao wako nje ya mradi na wanapaswakutafuta klabu mpya.”

Anasema Juventus iko tayari kufanya biashara na klabu nyingine kwa ajili ya wachezaji hao, lakini kwa sasa Chiesa akiwa ndiye mchezaji maarufu zaidi kwenye orodha ya wale wanaotakiwa kuondoka, kwani ni kama nembo ya timu hiyo aliyojiunga nayo akitokea Fiorentina miaka minne iliyopita.

Picha za mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 zilivutia na kushawishi wakati anajiunga na Juventus, lakini amepitia wakati mgumu kutokana na majeraha, na Juventus wanataka kumuuza katika dirisha hili badala ya kumuacha mkataba wake hadi umalizike msimu ujao ambapo ataondoka bure.

Motta anaongeza: “Ndio, kutokuwepo kwa Chiesa kunahusiana na soko. Hii ni kwa Federico na wengine waliosalia Turin isipokuwa Miretti (Fabio) ambaye ni majeruhi.”

Staa mwingine anayetakiwa kuondoka ni Weston McKennie aliyekuwa ameunganishwa na dili la uhamisho kwenda Aston Villa kama sehemu ya uhamisho wa Douglas Luiz. Hata hivyo, kocha wa Villa, Unai Emery alipendezwa zaidi na Samuel Iling-Junior na Enzo Barrenchea, hivyo MacKennie kubaki. Tayari Iling-Junior na Barrenchea wameshatua Villa wakitokea Juventus.

Mchezaji mwingine wa timu hiyo, Arthur Melo alikuwa na msimu mzuri uliopita wa mkopo akiichezea Fiorentina baada ya kucheza Liverpool kwa mkopo pia katika msimu wa 2022-23. Nyota huyo anatajwa kuwa katikati ya kubaki au kuondoka Turin.

Kwa maingizo mapya, tayari Juventus imemsajili Khephren Thuram kutoka Lille na Juan Cabal aliyetua akitokea Verona msimu huu na wanaripotiwa kuwa kwenye mbio za kumchukua Jean-Clair Todibo, ambaye alikuwa lengo la zamani la Manchester United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live