Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jurrien Timber mambo safi Arsenal

Jurrien Timber Jurrien Timber mambo safi Arsenal

Sat, 1 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Arsenal imefikia makubaliano ya uhamisho wa beki kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Ajax, Jurrien Timber, kwa mujibu wa 90minutes.

Washika Bunduki hao tayari wamethibitisha kumsajili Kai Havertz kutoka Chelsea wiki hii kwa dili la thamani ya zaidi ya Pauni milioni 65, huku wakiwa wamekubali uhamisho wa rekodi ya England na West Ham kwa Declan Rice ambaye atajiunga nao kwa pauni milioni 105.

Ofa ya ufunguzi ya Arsenal ya euro milioni 35 kwa Timber ilipungukiwa na bei ya Ajax ya ya euro milioni 60. 90minutes inaelewa kuwa ada ambayo imekubaliwa itaifanya Arsenal kulipa euro milioni 42 ya awali, ikiongezwa kwa euro milioni 5 katika nyongeza.

Maslahi binafsi tayari yamekubaliwa na kambi ya Timber na sasa inaweza kufungua njia ya kukamilika kabla ya wikendi.

Inaonekana tumaini kuu la Timber anayecheza upande wa kulia ni kwamba atacheza sambamba na Oleksandr Zinchenko.

Huku rekodi ya Rice ikiwa tayari kuthibitishwa, dili la Timber litamweka nafasi ya 10 kwenye orodha ya muda wote ya ada ya uhamisho iliyolipwa zaidi ya Arsenal, mbele ya Alexis Sanchez, Shkodran Mustafi na Granit Xhaka, lakini chini ya Mesut Ozil, Gabriel Jesus, Thomas Partey na Alexandre Lacazette.

Chanzo: Dar24