Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jurgen Klopp ukimzingua, anakuzingua

Jurgen Klopp 4 Jurgen Klopp.

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Masta Jurgen Klopp anaicha England, lakini moja kati ya mambo yatakayokumbukwa daima kuhusu yeye ni majibizano na ugomvi aliowahi kuujenga na waandishi ama mashabiki kwenye media.

Klopp sio mvumilivu kwenye jambo au mtu yeyote anayeisema vibaya timu yake. Huwa anachukua uamuzi wa kumchana papo hapo.

Haya hapa matukio matano aliyoyafanya mbele ya vyombo vya habari, ikiwamo kugombana na waandishi waliomuhoji kuhusu kuita fainali za Afcon ni mashidano madogo.

Kwenye mchezo wa Debi ya Merseyside, Desemba, 2017, Klopp akiwa kwenye msimu wake wa pili Liverpool waliikaribisha Everton Anfield mchezo wa Ligi Kuu England.

Baada ya kupata bao la kuongoza la Mohamed Salah, Everton ilisawazisha kwa penalti baada ya Dejan Lovren kufanyiwa faulo na Dominic Calvert-Lewin.

Baada ya mechi Klopp mwandishi Patrick Davison alimuuliza Klopp juu ya tukio hilo na alijibu: “Mkono ulikuwa kama hivi kwenye mgongo wake (Huku akionyesha ishara), kama unafikiri ni penalti sawa, sema, amua wewe ilikuwa ni penalti ni kweli unafikiri ilikuwa ni penalti kwa mtazamo wako?”

Davison akajibu kwa kusema ni kweli Lewin hakusukumwa sana lakini yeye anaamini ilikuwa ni penalti.

Klopp akacheka kisha akamwambia hawezi kuendelea kufanya mahojiano na yeye kwa sababu hajui chochote kuhuusu soka. “Nataka kuzungumza tu na watu ambao wana fahamu vizuri kuhusu soka, tunaweza kuacha kuzungumza? Kwa sababu sijisikii na naona hauna maswali ya kuniuliza.”

MAJIBIZANO NA KELLY Klopp amekuwa akilaumu juu ya muda wa mechi za England hasa za Jumamosi na anaona ni mapema sana. Takwimu zinaonyesha Liverpool ni miongoni mwa timu zinazocheza mechi zake nyingi siku hiyo na hali inayosababisha wasiwe na muda mwingi wa kupumzika, hususan katika misimu ambayo timu hii inashiriki michuano ya kimataifa.

Mara moja waliwahi kupoteza mechi dhidi ya Brighton na baada ya mechi Klopp alipohojiwa na mtangazaji wa BT Sport, Des Kelly alimlaumu kwa kitendo cha televisheni yao kuwapangia mechi ya mapema. Mtangazaji huyo alimkumbusha Klopp timu yake ilikubali mkataba wa mamilioni ya Pauni ambao uliipa BT Sport haki wachague muda wa mechi kuanza.

SAKALA LA AFCON Hapa alijichanganya kwa waandishi wa habari wa Afrika. Kwenye moja ya mikutano na waandishi wa habari alisema: “Januari kutakuwa na mashindano madogo barani Afrika, Asia pia wanayo na hata Amerika ya Kusini, yote haya ni mazuri, nayasubiri kwa hamu.”

Waandishi na mashabiki wa soka Afrika wakamshambulia kwa kumwambia amewadharau na kuwatukana wachezaji wake wanaoenda kwenye michuano hii, mashabiki na Afrika kwa jumla.

Katika utetezi wake Klopp alisema hakumaanisha hivyo watu walivyotafsiri na akakataa kuomba msamaha kwa kauli zake hizo.

HASIRA KWA MWANDISHI Baada ya kuiwezesha Liverpool kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu England wakati ligi ikiwa inaendelea msimu wa 2019/20, Majogoo hawa walienda kucheza dhidi ya Manchester City na wakapoteza kwa kichapo cha mabao 4-0.

Baada ya mechi wachambuzi wengi walidai Liverpool ilikuwa inacheza bila presha kwa kujua imechukua ubingwa na ndiyo maana ikapoteza mechi hiyo.

Katika mahojiano baada ya mechi Klopp alisema: “Tulikuwa tumeelekeza akili zetu hapo, unaniuliza swali hili mara ya pili, kama unataka kuandika akili yetu haikuwa kwenye mechi ndio maana tumefungwa, sawa tu, lakini nimeshakwambia haipo hivyo,” alisema Klopp kwa hasira.

KUMZINGUA KEANE Septemba, 2020, wakati Liverpool inapambana kutetea taji lao, ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Arsenal na baada ya mechi Roy Keane akiwa studio alisema timu hiyo ilikuwa ikicheza taratibu sana.

Klopp akasikia na alipoulizwa kuhusu mechi kwa jumla alisema: “Hivi nimemsikia vizuri Keane, amesema tulikuwa tunacheza taratibu leo, sina hakika kama nilimsikia vizuri, lakini labda mechi nyingine sio hii, samahani leo hatukuwa tunacheza taratibu.”

Keane akajibu anaheshimu sana kiwango kilichoonyeshwa na Liverpool kwenye mechi hiyo na itakuwa Klopp alimsikia vibaya, Klopp akasema ataenda kutazama tena video ya Keane akiongea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live