Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jurgen Klopp amwaminia Nuri Sahin ile mbaya

Klopp X Nuri Sahin Jurgen Klopp amwaminia Nuri Sahin ile mbaya

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anaamini bosi mpya wa Borussia Dortmund, Nuri Sahin atakuja kuwa kocha wa viwango vikubwa kwenye mchezo huo wa soka la dunia.

Sahin, ambaye aliichezea Dortmund kuanzia 2005 hadi 2011 kisha kuanzia 2013 hadi 2018, alitangazwa kuwa kocha mpya wa miamba hiyo ya Bundesliga. Taarifa hiyo imemvutia kocha wa zamani wa BVB, Klopp, ambaye anaamini Sahin, 35, atakwenda kupata mafanikio makubwa kwenye kikosi hicho na kuwa kocha bora kabisa duniani.

“Katika umri wa miaka 35, Nuri ni kocha kijana sana, lakini nami nilikuwa hivyo,” alisema Klopp.

“Ninaamini kabisa baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa akiwa mchezaji, bila shaka atakwenda kuwa kocha bora kabisa. Namtakia kila la heri BVB.”

Sahin, ambaye pia aliwahi kuichezea Real Madrid na kidogo Liverpool, alichukua mikoba ya kuinoa Dortmund kutoka kwa kocha Edin Terzic, ambaye amefutwa kazi na timu hiyo baada ya kumaliza nafasi ya tano kwenye msimamo wa Bundesliga, licha ya kwamba aliifikisha timu hiyo kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuchapwa na Real Madrid uwanjani Wembley mwanzoni mwa mwezi huu.

Klopp anaamini staa huyo wa zamani wa kimataifa wa Uturuki atapata mafanikio makubwa huko Dortmund huku akifichua uhusiano mzuri uliopo baina yao, ambao ulijengeka walipokuwa pamoja kwenye kikosi hicho cha Signal Idunna Park.

Sahin aliichezea Dortmund mechi 274 na alirejea kwenye kikosi hicho Januari mwaka huu kwenda kuwa kocha msaidizi. Kipindi chake bora kabisa Sahin kwenye kikosi hicho cha Westfalenstadion ni wakati alipokuwa chini ya kocha Klopp, kabla ya kwenda Werder Bremen alikoshinda taji la Bundesliga msimu wa 2010/2011 na kuchaguliwa mchezaji bora wa msimu kwenye Bundesliga mwaka 2011.

Chanzo: Mwanaspoti