Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Juma Mgunda akubali kubebeshwa zigo la lawama

Kikoisi Simba SC 1140x640 Juma Mgunda akubali kubebeshwa zigo la lawama

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: Dar24

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amekubali kubeba lawama zote, kufuatia kikosi chake kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC jana Alhamisi (Oktoba 27).

Azam FC walikua wenyeji wa mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuanzia saa moja usiku, huku bao la ushindi likifungwa na Mshambuliaji wao kutoka nchini Zimbabwe Prince Mpumelelo Dube.

Mgunda amekiri kupokea matokeo hayo na kusisitiza ni sehemu ya mchezo wa soka, ambao siku zote umekua na matokeo ya aina tatu kufungwa, kushinda na kutoa sare.

Kocha huyo kutoka Mkoani Tanga amesema yote yaliyotokea Uwanja wa Benjamin Mkapa jana Alhamis (Oktoba 27) hadi kupelekea kikosi chake kupoteza, yanapaswa kuelekezwa kwake kama Kaimu Kocha Mkuu na sio kwa Wachezaji.

“Ninapaswa kuwajibishwa mimi kama Kocha Mkuu, wachezaji wote waliocheza dhidi ya Azam FC ni wa Simba SC na mimi ndio niliidhinisha wacheze, kwa hiyo kukosea kwao na kupatia kwao mimi ndio napaswa kulaumiwa.

“Nimeyapokea matokeo ya mchezo huu kama sehemu ya Soka, tumepoteza kwa sababu hatukuwa bora kama ilivyokua kwa wenzetu, tunajipanga kwa mchezo ujao, ili tuweze kurejea katika njia ya ushindi.

“Mapungufu yaliyopelekea tukapoteza na kushindwa kutumia nafasi tulizozitengeneza ninakwenda kuyafanyia kazi katika Uwanja wa mazoezi ili turejee kwenye ubora katika mchezo wetu unaofuata,” amesema Kocha Juma Mgunda.

Simba SC itakua mwenyeji wa Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro siku ya Jumapili (Oktoba 30), Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku.

Simba SC imepoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu, inaendelea kubaki na alama 14 sawa na Azam FC iliyosogea hadi nafasi ya tatu, huku Young Africans ikiwa kileleni kwa kufikisha alama 17, ikifuatiwa na Mtibwa Sugar yenye alama 15.

Chanzo: Dar24