Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio atangazwa Kocha Mkuu Singida FG, apewa 10 za mwisho

Jamhuri Kihmelu Julio.jpeg Julio apewa 10 za mwisho Singida FG

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida Fountain Gate FC imemtambulisha Jamhuri Kiwelu (Julio) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo hadi mwisho wa msimu baada ya wiki iliyopita kuvunja benchi zima la ufundi lililokuwa chini ya Thabo Senong.

Singida FG imeamua kumpa kazi Julio baada ya kutoridhishwa na matokeo ya timu yao ilipokuwa chini ya Senong.

Singida FG kwa sasa inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuvuna pointi 21, pointi 28 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Yanga.

Timu hiyo imebakiza mechi 10 kuamua hatima yao kama itaendelea kubaki kwenye Ligi Kuu au itaporomoka kwenda kwenye Championship msimu ujao.

Wengine walioongezwa kwenye benchi hilo la ufundi ni pamoja na aliyekuwa kocha wa muda wa timu hiyo Ngawina Ngawina ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi na Ally Mustapha ‘Barthez’ kuwa kocha wa makipa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: