Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio aleza sababu Ngorongoro kufungwa

A9c44b7cc157d9313d025e18dcbc23f5 Julio aleza sababu Ngorongoro kufungwa

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADA ya timu ya taifa ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kufungwa mabao 4-0 na Ghana kwenye michuano ya AFCON, kocha wa kikosi hicho, Jamhuri Kihwelo 'Julio',amesema walipoteza mchezo kutokana na wachezaji kushindwa kutumia vizuri nafasi za kufunga lakini a ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye michezo ijayo.

Ngorongoro Heroes ambayo ipo Kundi C inashiriki kwa mara ya kwanza mashindano hayo yanayofanyika Mauritania.

''Timu imejitahidi imecheza vizuri kwani tulitawala mchezo, lakini nafasi tulizozipata hatukuweza kuzitumia vizuri, pamoja na kuwaheshimu Ghana sio kwamba wametuzidi isipokuwa walipata nafasi na kuzitumia sisi hatukuzitumia vizuri.”

''Tuna amini mechi nyingine tutafanya vizuri hata leo (juzi) hatukufanya vibaya sana, nawapongeza wachezaji ila ugeni wa mashindano ndio uliochangia kupoteza kwa sababu wenzetu wana uzoefu ndio maana wameweza kutumia nafasi walizopata,” alisema.

Mchezo mwingine wa kundi hilo timu ya taifa ya Morocco iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya taifa ya Gambia.

Ghana ndio inaongoza Kundi C ikiwa na pointi tatu sawa na Morocco ila zikitofautiana kwa mabao ya kufunga, Gambia inashika nafasi ya tatu ikiwa haina pointi sawa na Tanzania inayoburuza mkia.

Mchezo unaofuta Tanzania itacheza na Gambia kesho na mchezo wa mwisho itacheza dhidi ya Morocco Februari 22.

Chanzo: habarileo.co.tz