Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio aipa masharti Azam

Azam Fc At Cecafa Tournament 1m9qh6jlr7u4v1obwuxjsym8sg Julio aipa masharti Azam

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelKOCHA na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' ameutaka uongozi wa Azam FC kufanya mambo mawili makubwa ili timu hiyo iwe na hadhi kubwa sawa na Simba, Yanga au kuzizidi.

Akizungumza katika Bonanza la Uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Azam FC, Julio amesema kuwa timu hiyo inatakiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na mashindano mengine itakayoshiriki pia kuhakikisha inapandisha hadhi ya Tamasha lake ililolianzisha kama ilivyo kwa Simba.

"Mimi nasikia uchungu sana pale Azam FC isipofanya vizuri kutokana na miundombinu waliyonayo lakini naamini watajipanga vizuri na msimu ujao wataleta ushindani na kufanya vizuri.

"Pia nauomba uongozi wa Azam uongeze bajeti ya fedha kwa tamasha hili (Tamasha la Siku ya Azam) ili lilete tija kama ambavyo Simba, tamasha lao linavyoleta tija," amesema Julio.

Katika hatua nyingine, Julio ambaye pia amewahi kuzinoa Mwadui FC na Dodoma Jiji FC, ameipongeza Azam FC kwa uzinduzi wa jezi mpya ambazo watazitumia msimu ujao.

Tamasha la maadhimisho ya Wiki ya Azam FC lilizinduliwa rasmi jana Jumapili Agosti 16, 2020 katika Uwanja wa Azam Complex ambapo lilipambwa na shughuli kubwa tatu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz