Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio achora ramani kubaki Ligi Kuu

Julio 1000x640 Julio achora ramani kubaki Ligi Kuu

Fri, 5 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati KMC ikihaha kukwepa kushuka daraja, kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ameanza kupiga hesabu za kushinda mechi tatu zilizobaki huku akionesha matumaini kwa vijana wake na morali waliyo nayo na kiu ya ushindi.

Julio aliyekabidhiwa majukumu ya kuiongoza timu hiyo hivi karibuni, tayari ameisimamia mchezo mmoja dhidi ya Dodoma Jiji na kuambulia kipigo cha bao 1-0.

Hadi sasa KMC ipo nafasi ya 14 kwa pointi 28 na imebakiza mechi tatu ikianza na Singida Big Stars, Mei 12 nyumbani kisha kusafiri kuzifuata Tanzania Prisons na kuhitimisha na Mbeya City.

Julio alisema licha ya kuanza vibaya ni matokeo aliyotarajia kutokana na ugeni aliokuwa nao lakini hali ya wapinzani wao Dodoma Jiji, hivyo kwa sasa haoni tena wakipoteza tena mechi yoyote.

Alisema kwa sasa akili na nguvu zao zipo kwenye mechi ijayo dhidi ya Singida BS, huku akieleza kuwa maandalizi waliyonayo ikiwamo mechi za kirafiki zinaongeza morali na kujiamini kwa vijana.

“Tumekuwa na maandalizi ikiwamo mechi ya kirafiki dhidi ya Azam tuliyopata sare ya 1-1, hiki ni kipimo kwetu katika mwendelezo wa kujiweka fiti na mechi ijayo dhidi ya SBS, tunahitaji ushindi michezo iliyobaki,”

“Mashabiki na wadau wote wa soka wa KMC, wawe na matumaini na timu yao kwa muda nilionayo kwa sasa naona mabadiliko mazuri ya kutia matumaini hatutaki hata play off,” alisema Julio.

Chanzo: Mwanaspoti