Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio abwaga manyanga Singida FG baada ya mechi mbili tu

Jamhuri Kihmelu Julio.jpeg Kocha Julio

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuiongoza Singida Fountain Gate FC kwenye michezo miwili, Kocha Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ameondoka kwenye kikosi hicho ambacho maskani yake kwa sasa ni jijini Mwanza.

Jana Julio aliiambia SportsXtra kuwa, kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa mapumziko ya Eid El Fitr lakini kuna mambo hayapo sawa kati yake ya Singida Fountain Gate lakini pindi yatakapokaa sawa atarejea kuendelea na majukumu yake.

“Nimerudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya siku kuu [Eid El Fitr] na kuna mambo yetu fulani hayajakaa sawa, yakishakaa sawa mambo mengine yataendelea.”

“Bwana mkubwa [Japheth Makau] alikuwa Afrika Kusini, tayari amerudi tutaangalia mambo yakikaa sawa mambo mengine yataendelea. Sisi makocha kazi yetu ni kufundisha na kupata maslahi.”

“Mimi nilikuwa niajiriwe tangu mechi ya Simba vs Singida Fountain Gate FC lakini kwakuwa tayari kulikuwa na kocha mwingine ameshaiandaa timu nikaamua nisiingilie mipango yake. Timu ikacheza na Simba japo ilipoteza lakini ilicheza vizuri hususan kipindi cha pili.”

“Mechi yangu ya kwanza nikiwa Singida Fountain Gate ilikuwa dhidi ya Namungo, tukafanikiwa kushinda, mechi ya pili ilikuwa ya FA dhidi ya Tabora United tukapoteza.”

“Mechi hiyo kwangu haikuwa na umuhimu mkubwa kwetu kwakuwa tuliangalia mazingira ya timu yetu yalivyo na kipaumbele chetu kwa sasa ni kuibakiza timu Ligi Kuu kama ambavyo wenyewe wanataka.”

Singida Fountain Gate FC inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Yanga siku ya Jumapili, Aprili 14, 2024 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live