Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio aanza mipango ya 5 bora Ligi Kuu

Jamhuri Kihmelu Julio.jpeg Julio aanza mipango ya 5 bora Ligi Kuu

Sat, 23 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya mapumziko ya wiki moja, kikosi cha Singida Big Stars kimerudi kambini kujiandaa na mapambano, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ akisisitiza yupo kwenye mipango mkakati ya kusaka Tano Bora ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu.

Kocha huyo maarufu nchini, amezitaja Yanga, Ihefu FC na Coastal Union kuwa ndio timu tishio kwenye mechi 10 zilizosalia kwao tangu akabidhiwe timu hiyo na kuiongoza kupata ushindi katika mechi ya kwanza dhidi ya Namungo wiki iliyopita walipoinyoa kwa bao 1-0.

Julio alisema licha ya uwepo wa mapambano magumu duru hili la pili kwa kila timu kusaka pointi tatu, kwa upande wake anapambana timu kumaliza kwenye nafasi ya tano za juu ikiwa ni mkakati wake kati ya mambo 10 aliyopewa mara alipokabidhiwa Singida iliyoweka maskani jijini Mwanza.

“Hizi mechi tisa ni nyingi japo zipo baadhi ya mechi ni za moto. Mechi na Yanga ya moto, hata ile ya Ihefu nayo si mchezo na kuna Coastal, lakini kwa vile mimi ni muumini wa maopambano naamini tutapata matokeo mazuri,” alisema beki na kocha wa zamani wa Simba aliyeongeza;

“Nasema timu hizo ni za moto hii ni kutokana na namna wanavyocheza na kuwa na mabadiliko makubwa ya vikosi vyao lakini hilo halinitishi nitawaandaa vijana wangu kuhakikisha wanaonyesha ushindani na kutafuta pointi tatu ili tuweze kufikia malengo.”

Akizungumzia mapumziko ya wiki moja licha ya timu kutokuwa na matokeo mazuri alisema ilikuwa ni lazima wapumzike ili kuwajenga kisaikolojia kwani mpira una matokeo matatu ata wangefanya mazoezi kipindi chote bado wangepoteza huku akisisitiza kuwa hakuna timu isiyo fungwa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: