Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba SC, Jamuhuri Kihwelu 'Julio' amesema kuwa kilichowabeba Yanga SC ni ubora uzoefu wa wachezaji wao tofauti na Namungo FC ndiyo maana maana wakashinda bao 1-0 na kuondoka na alama tatu katika Dimba la Azam Complex.
Julio ambaye amewahi kuifundisha Namungo FC amesema kuwa Yanga haijabadilika sana na ile ya msimu uliopita ndiyo maana imekuwa na mwendelezo wa kupata matokeo chanya kwani wachezaji wake wengi wamezoeana.
Takwimu hazikumbeba, ufundi wa mchezaji mmoja wa Namungo na Yanga haufanani lakini bado alimuliza maswali magumu kocha Miguel Gamondi siku ya jana, Cedric Kaze alikosa wachezaji wakuimaliza mechi.
Akizungumzia mchezo huo, Julio amesema; “Yanga wancheza vizuri kwa sababu wamekaa muda mrefu na wameingiza watu wachache ambao wanakuja kuleta chachu timu ifanye vizuri tatizo la Watanzania wana haraka.
“Watu wanataka mtoto azaliwe leo atembee hilo haliwezekani anayeweza kuzaliwa na kutembea ni mtoto wa mbuzi pekee," amesema Kocha Jamuhuri Julio.