Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio: Simba ifukuze wachezaji wote abaki Kibu pekee

Kibu D KIBU DENGA.jpeg Julio: Simba ifukuze wachezaji wote abaki Kibu pekee

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Singida Fountain Gate FC, Jamhuri Kiwelu (Julio) amesema kuwa imefika wakati klabu ya Simba inatakiwa kuwaondoa kikosini nyota wao wote na kuwaacha wanaojituma tu kama Kibu Denis kisha kuleta wachezaji wengine ambao wapo tayari kuipambania timu.

Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa watani zao Yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi Aprili 20, katika Dimba la Mkapa.

“Ni almost timu yote wanatakiwa wafanye reshuffle timu nzima. Mtu kama timu unamuona anajituma lakini wengine huwaoni.

"Tuwaondoe tupate washambuliaji wazuri, viungo wazuri na mabeki wazuri. Mabeki wa Simba wanacheza wide, pale kati tunaacha nafasi, ukikutana na watu wa kasi wanatushambulia," amesema Julio.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live