Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Julio: KMC FC itabali Ligi Kuu 2023/24

Image 488.png Julio: KMC FC itabali Ligi Kuu 2023/24

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa KMC FC Jamhuri Kihwelo Julio’ amesema bado kikosi chake kina nafasi ya kubaki Ligi Kuu, licha ya kuwa nyuma kwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Play Off.

KMC FC juzi Jumanne (Juni 13) ilicheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza ugenini jijini Mbeya, na sasa najiandaa kwa mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa jijini Tanga Jumapili (Juni 18).

Kocha Julio amesema mchezo wa Mkondo wa kwanza ulikuwa mgumu kwa sababu kila timu ilitaka ushindi ili kujibusuru kushuka daraja, lakini kitendo cha kupata bao moja kimewafanya wawe na imani kuwa wanaweza kupindua matokeo nyumbani.

“Mechi ilikuwa ngumu, kila timu ili cheza kwa nguvu ikiwa na nia ya kutaka kujinusuru, hili bao moja linaweza kusababisha mimi kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano,” amesema Julio

Akiizungumzia mechi yenyewe amesema kipindi cha kwanza wachezaji wake hawakuwa na utulivu kutokana na presha ya mchezo wenyewe, lakini alipofanya mabadiliko kipindi cha pili, kila kitu kikabadilika.

“Kipindi cha kwanza vijana wangu hawakuwa na utulivu kwa sababu ya presha ya mechi yenyewe, kipindi cha pili nilifanya mabadiliko vijana wangu wakatulia lakini kwa bahati mbaya tumepoteza, tukijipanga vizuri tutabaki Ligi Kuu,” amejinasibu

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Mbeya City, Abdallah Mubiru amelia na safu yake ya ushambuliaji, akisema kuwa ilitakiwa kufunga mabao mengi.

“Wachezaji wamefanya kila kitu walichoweza na uwezo ndiyo umefikia pale, tumeklosa kufunga magoli tu, kwenye soka ndiyo maana timu kubwa zinakwenda kununua masstraika kwa gharama kubwa, angalia tunacheza vizuri lakini ufungaji ndiyo tatizo, unaweza kufundisha sana mazoezini jinsi ya kufunga, lakini wakati mwingine kuweka mpira ndani ya wavu ni kipaji cha uwezo wa mtu binafsi wa mchezaji,” amesema

Hata hivyo amesema watakwenda jijini Dar es salaam kupambana kwenye mechi ya marudiano kuhakikisha wanabaki Ligi Kuu.

Mechi ya pili inatarajiwa kuchezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga ambako KMC imeamua kulipeleka pambano hilo huko.

Mshindi wa jumla atabaki Ligi Kuu na aliyefungwa atakwenda kucheza mechi nyingine ya mchujo dhidi yimu ya Championship ya Mashujaa FC ya Kigoma.

Chanzo: Dar24