Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jukwaa la mkesha lachelewesha mechi ya Yanga kwa Mkapa

Screenshot 20221217 220704 Facebook Jukwaa la mkesha lachelewesha mechi ya Yanga kwa Mkapa

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati inasubiriwa kupigwa mechi ya Ligi Kuu baina ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania saa 1:00 usiku huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, shughuli za kutoa jukwaa lililofanyiwa mkesha wa maombi jana Ijumaa bado zinaendelea.

Mechi hiyo ilitakiwa ianze saa 1:00 usiku ila hadi sasa bado wachezaji hawajaanza kuingia uwanjani hapo kutokana na shughuli ya kuondooa jukwaa bado zinaendelea.

Sababu ya kuchelewa kwa mechi hiyo ni kutokana na jukwaa hilo ambalo lilitumika katika mkesha wa maombi janakuwa katikati ya sehemu ya kuingilia wachezaji.

Hata hivyo polisi wameonekana kusogea eneo hilo, baada ya muda waliokuwa wanafungua machuma ya jukwaa hilo kuondoka.

Baada ya dakika moja walionekana wafanyakazi hao kurudi tena, jambo ambalo lilianza kupigiwa kelele na mashabiki hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live