Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jude Bellingham anazidi kujipata

Adsfdfdgfg Jude Bellingham anazidi kujipata

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Umepita msimu mmoja tangu Jude Bellingham ajiunge na Real Madrid, kila uchao amezidi kuwika na kuendelea kuwa mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha England na Madrid kwenyewe.

Lakini mbali ya kuzidi kuimarika kiuchezaji, staa huyu pia amezidi kuimarika kimfuko, kwani amekuwa akisaini madili mapya na kuzidi kutajirika.

Leo tumekusogezea uone jinsi jamaa alivyoongeza utajiri wake ndani ya mwaka baada ya kutua Madrid.

ANAPIGAJE PESA

Mshahara wake ndani ya Madrid ni Pauni 220,000 kwa wiki ambao hufikia Pauni 11 milioni kwa mwaka.

Pia anapata pesa kupitia mikataba ya udhamini na makampuni mbalimbali.

Kwa sasa yupo chini ya Adidas ambao wanamlipa kwa kutangaza viatu vyao, lakini hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba Nike inataka kumchukua na kumpa ofa nono zaidi.

Ofa hiyo ya Nike inaweza kuwa ya mkataba wa maisha.

Fundi huyu pia ni balozi wa kampuni ya mavazi ya Kim Kardashian iitwayo SKIMS ambapo kwa mwaka anapata zaidi ya Dola 2.5 milioni.

Ameingia pia mkataba na kampuni ya Louis Vuitton inayojihusisha na kudizaini nguo, mabegi na manukato.

Kiujumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 40 milioni na mbali ya kampuni tajwa hapo juu, staa huyu pia ni balozi wa kampuni nyingine kama Lucozade, SWM Exclusive na EA Sports.

Alipokuwa Dortmund, aliriripotiwa kuwa na utajiri usiozidi Pauni 5 milioni.

MAGARI

Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti mbalimbali staa huyu hana magari mengi na yale ambayo ameonekana nayo kwa sasa ni mawili la kwanza ni BMW XM alilopewa mara tu baada ya kutua Madrid, gari hii ina thamani ya Dola 162,000. Pia anamiliki Mercedes Benz

MJENGO

Kwa sasa anaishi huko La Finca, Madrid, Hispania yeye na familia yake katika mjengo ambao wamepangiwa na Madrid ikiwa ni sehemu ya mkataba wake.

Mara nyingi kila anapohama huwa anasafiri na baba, mama na mdogo wake wa kiume.

MSAADA KWA JAMII

Mwaka 2021, akishirikiana na Mustard Seed Project alijenga zaidi ya madarada 200 na kutoa vifaa vya michezo kwa watoto waishio katika mazingra magumu huko Mombasa, Kenya.

Vifaa hivho zilikuwa ni udhamini kutoka kwa kampuni ya Adidas ambayo yeye ni balozi wake.

BATA NA MAISHA BINAFSI

Anadaiwa kuwa katika uhusiano na mwanamitindo na modo Laura Celia Valk, ambaye ni raia wa Uholanzi, inaelezwa wawili hawa walianza mahusiano yao mwaka jana muda mchache baada ya Jude kujiunga na Madrid. Hadi sasa bado hawajaweka wazi mahusiano yao.

Anapokuwa nyumbani jamaa sio mtu wa bata sana kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Kiingereza.

Chanzo: Mwanaspoti