Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jude Bellingham ajimwambafai Real Madrid

Jude Bellingham To Madrid Jude Bellingham

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo Mshambuliaji Jude Bellingham amesema amekuwa bora mara 10 kuliko alivyokuwa msimu uliopita katika Klabu ya Borussia Dortmund baada ya kuendelea na maisha yake mazuri akiwa Real Madrid kwa mabao mawili na kusaidia katika ushindi wa 3-1 kwenye dhidi ya Almeria, mwishoni mwa juma lililopita.

Bellingham amezoea maisha ya Madrid haraka tangu uhamisho wake wa Euro Milioni 103 kutoka klabu hiyo ya Bundesliga, akifunga bao katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Athletic Club mwishoni mwa juma lililopita kabla ya mabao mawili Jumamosi kwenye Uwanja wa Power Horse.

“Nadhani mimi ni mchezaji bora mara 10 kuliko msimu uliopita,” Bellingham aliiambia Real Madrid TV.

“Ninajifunza kutoka kwa wachezaji hawa. Kiwango cha hapa ni cha juu sana.

Sergio Arribas aliiweka mbele Almeria mapema kabla ya Bellingham kusawazisha dakika ya 19 na kisha kuiweka Madrid mbele kwa bao la kichwa, kabla ya Vinicius Junior kufunga la tatu.

“Niliona Real Madrid ikirejea mara nyingi kwenye TV nilipokuwa mtoto,” alisema Bellingham.

“Nakumbuka nilifikiri hawataweza na mwisho walifanya hivyo, sasa nipo na naona, sikuwahi kufikiria kuwa tutapoteza, niliangalia nyuso za wachezaji na hakukuwa na hofu.”

Baada ya kufunga bao lake la kwanza msimu huu, Vinicius alisema anatumaini ushirikiano wake na Bellingham unaweza kufikia lile aliloshiriki na mchezaji mwenzake wa zamani, Karim Benzema.

Chanzo: Dar24