Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jude Bellingham aingia anga za Ronaldo Real Madrid

Jude Bellingham La Liga Jude Bellingham

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jude Bellingham aliifungia tena goli Real Madrid katika ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Girona, Jumamosi, Septemba 30 na kufikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya miaka 14 na kusaidia timu yake kurejea kileleni mwa LaLiga.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amelingana rekodi na Ronaldo kwa kufunga mabao Sita (6) katika mechi Saba (7) za kwanza, sawa na Ronaldo ambaye katika msimu wake wa kwanza 2009/10 akiwa na Los Blancos alifanya hivyo.

Tangu Muingereza huyo ahamie Bernabeu akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho itakayoongezeka hadi kufika pauni milioni 115, zaidi ya TZS Bilioni 350 amekuwa na mwanzo mzuri sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live