Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jude Bellingham: Ninamkubali sana Zidane

Zidane Jude Age 620.png Jude Bellingham

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mpya wa magwiji wa jiji la Madrid ‘Real Madrid’, Jude Bellingham amefichua kuwa amekuwa akimkubali kiungo wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane ndiyo maana akakubali kuchukua jezi yake namba 5.

Bellingham ametua ndani ya Real Madrid kwa dau la euro milioni 103 na baada ya kutambulishwa na timu hiyo akakabidhiwa jezi namba 5 ambayo ataivaa akiwa hapo jezi ambayo iliwahi kuvaliwa na Zidane wakati akiichezea timu hiyo.

Kiungo huyo, 19, amekabidhiwa jezi hiyo kutokana na jezi anayoipenda kuivaa namba 22 kuvaliwa na beki Antonio Rudiger ndani ya kikosi hicho.

Akizungumza kwenye utambulisho wake, Bellingham alisema: “Nimesema mara nyingine kwenye mahojiano namna gani namkubali Zinedine Zidane, heshima aliyokuwa nayo hapa akiwa na namba hii.

“Lakini nitajaribu kuwa Jude, lakini amekuwa na heshima kubwa akiwa hapa. Namba 22 ina maana kubwa kwangu na kwenye moyo wangu, bado ni namba 22 mwenye namba 5 mgongoni.

“Najua jezi Madrid pekee imekuwa na presha kubwa, kwangu mimi ni jambo kubwa lakini hii itanifanya niwe mchezaji mkubwa. Inawezekana nikaongeza heshima ya jezi hii (namba 5) badala ya kufika ile yake,” alisema Bellingham.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live