Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joto la Ballon d’Or kila staa ataja mshindi wake

Ballon Pic Baadhi ya wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon Di'or

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Muda sio mrefu, atajulikana mshindi wa Ballon d’Or 2021.

Swali lililopo, je Lionel Messi atanasa tuzo ya saba ya Ballon d’Or?

Je, Robert Lewandowski atashinda tuzo aliyostahili kushinda mwaka jana?

Swali jingine, je Cristiano Ronaldo atashinda kulingana na Messi kwenye kushinda Ballon díOr?

Je, Jorginho atamshangaza kila mtu?

Maswali yote hayo yatapata majibu ndani ya wiki chache zijazo. Kura kutoka kwa makocha na manahodha wa timu za taifa zimeshapigwa na kinachosubiriwa ni matokeo tu. Lakini, hilo halina maana kwamba litazuia watu kutoa maoni yao.

Katika kuelekea kwenye sherehe za tuzo hizo, mastaa wengi waliulizwa wanadhani ni nani atashinda tuzo hiyo bora kabisa kwa mchezaji mmoja mmoja kwenye soka la dunia. Na hiki ndicho walichosema mastaa hao, wakiwachangua wachezaji wanaodhani wanastahili kushinda.

Ronaldo: Karim Benzema

“Bila ya shaka, chaguo langu kwenye Ballon d’Or ni Benzema. Mshambuliaji bora kabisa, amekuwa moto kwa zaidi ya miaka 10 na ni bingwa zaidi ya yote,” alisema Ronaldo.

Giorgio Chiellini: Jorginho

“Natumaini atashinda Ballon d’Or kwa sababu ni rafiki yangu na nadhani tuzo hiyo ni yangu kama Mtaliano. Alikuwa mtu muhimu kwenye mechi zetu. Nilimtambua Jorginho kama mchezaji bora baada ya kufanya mazoezi naye mara mbili tu,” alisema Chiellini.

Kevin De Bruyne: Robert Lewandowski

“Kwa kuangalia miaka miwili iliyopita kwa sababu mwaka jana tuzo hazikufanyika, ningependa tuzo ya Ballon d’Or ibebwe na Lewandowski,” alisema supastaa wa Manchester City, Kevin De Bruyne.

Gerard Pique: Lionel Messi

“Ballon d’Or? Kama watafuata vigezo vya kushinda tu, basi Messi atashinda. Kama wataamua kumpa mchezaji bora duniani, Messi atashinda,” alisema Gerard, ambaye aliwahi kucheza pamoja na Messi huko Barcelona.

Zinedine Zidane: Karim Benzema

“Karim yupo mawinguni,” alisema Zidane na kuongeza. “Ningempa Ballon d’Or. Anastahili. Ni mchezaji wa aina yake, nilipata heshima kubwa sana kumnoa mazoezini. Anafahamu kitu cha kufanya ndani ya uwanja. Yupo juu.”

Marco Verratti: Jorginho au Lionel Messi

“Chaguo kati ya Jorginho na Messi ndilo litakaloshinda,” alisema Verratti. “Kama tutaamua kumpa mtu aliyeshinda kila kitu Ulaya, basi ni Jorginho. Kama tunataka mtu mwenye nguvu, mburudishaji kwa mashabiki, basi ni Messi.”

Maurcio Pochettino: Lionel Messi

Kocha wake huko Paris-Saint Germain alisema: “Ni Messi. Na hata kama sijamnoa Messi, ningesema Messi. Bila ya shaka. Lewandowski anaweza kuwa wa pili na namba tatu namuweka Cristiano.”

Roberto De Zerbi: Karim Benzema

“Ni Benzema haina utata.Kwa upande wangu, kwa miaka yote ndiye mshambuliaji wangu bora. Nje ya Lewandowski, namchagua Benzema,” alisema kocha huyo wa Shakhtar Donetsk, Roberto De Zerbi.

Pedri: Lionel Messi

“Hicho ni kitu ambacho hakipo juu yangu kukiamua, nina hakika watu ambao wataamua basi watampa yeye ndiye anayestahili. Kama nitafanya uamuzi mwenyewe, basi siku zote Leo ni bora kwangu,” alisema kinda huyo wa Barcelona.

Rafael Nadal: Karim Benzema

“Namkubali sana kama mchezaji kutokana na jinsi anavyojitolea uwanjani hasa ukizingatia na umri wake. Namtakia kila la heri na naunga mkono ashinde 2021 Ballon d’Or,” alisema Nadal, staa wa tenisi juu ya tuzo ya soka.

Rafael Marquez: Robert Lewandowski

“Bora wa muda wote ni Pele, licha ya kwamba sijawahi kumwona akicheza. Na mshindi wa Ballon d’Or wa mwaka huu ni Lewandowski. Kama atakuwa si yeye, basi nitachagua mmoja kati ya Leo Messi na Benzema, ni ngumu kumchagua mmoja tu baina yao,” alisema Marquez

Iago Aspas: Robert Lewandowski

“Nampenda sana Benzema, lakini nampa tuzo hiyo Lewandowski,” alisema straika wa Celta Vigo, Aspas.

Ronald Koeman: Lionel Messi

“Messi ni mshiriki mkuu wa tuzo hizi za mwaka huu akiwa ameshinda Copa America. Kwa upande wangu, ni mtu anayepewa nafasi kubwa ya kushinda Ballon d’or mwaka huu,” alisema kocha huyo wa zamani wa Barca, Koeman.

Julian Nagelsmann: Robert Lewandowski

Kocha wa Bayern Munich alisema. “Alistahili kushinda Ballon d’Or mwaka jana, hivyo kwa upande wangu nadhani anastahili kushinda pia mwaka huu kutokana na ukweli kwamba amecheza kwa kiwango bora kabisa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululuzo.”

Chanzo: Mwanaspoti