Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua Zirkzee avutiwa kasi Old Trafford, Emirates

Skysports Joshua Zirkzee Bologna 6510864 Joshua Zirkzee

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United inataka kuipiku Arsenal katika vita ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee, 23, ambaye katika mkataba wake kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa Pauni 34 milioni.

Zirkzee anawindwa na vigogo hawa kwa sababu alifanya maajabu katika Ligi Kuu Italia msimu uliopita.

VIGOGO wa Chelsea wameiambia Bayern Munich, hawanaa mpango wa kumuuza beki wao raia wa England, Levi Colwill, 21, katika dirisha hili.

Bayern inamwangalia Levi kama chaguo la kwanza na kama itamkosa ndio itahamia kwa Jonathan Tah ambaye imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wake ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kumnasa.

CHELSEA inataka kumsajili straika wa Aston Villa na Colombia, Jhon Duran, 20, kwenye dirisha hili ikiwa ni mwaendelezo wao wa kutaka kujenga timu kupitia wachezaji vijana.

Duran mwenye umri wa miaka 20, msimu uliopita alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao manane. Mkataba wa mshambuliaji huyo mwenye kipaji unamalizika mwaka 2028.

WEST Ham inaripotiwa kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumsajili straika wa AS Roma, Tammy Abraham ambaye pia anahitajika na Aston Villa na Tottenham.

Tammy anataka kuondoka Roma ili kubadilisha upepo kwa sababu anapitia wakati mgumu kwa msimu wa pili mfululizo. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

KOCHA mpya wa Bayern Munich Vincent Kompany amependekeza jina la beki wa Liverpool, Joe Gomez, 27, ambaye anahitaji asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo lao la ulinzi.

Gomez anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kukubali kutua kwa vigogo hawa maarufu kama Bavarians.

WEST Ham ipo tayari kumwachia beki wake raia wa Ufaransa, Kurt Zouma, 29, katika dirisha hili.

Zouma ambaye msimu uliomalizika alicheza mechi 33 za michuano yote, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Licha ya kuonyesha kiwango bora chini ya kocha aliyepita David Moyes, taarifa zinaeleza kocha mpya Julen Lopetegui hana mpango wa kumtumia.

ARSENAL imepanga kumuuza beki wake raia wa Scotland, Kieran Tierney kwa bei ya hasara katika dirisha hili.

Kwa mujibu wa tovuti ya Football Insider, Arsenal inahitaji ofa ya Pauni 15 milioni.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Katika msimu uliomalizika alicheza mechi 27 za michuano yote.

Chanzo: Mwanaspoti