Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joshua Kimmich kucheza England

Joshua Kimmich Joshua Kimmich kucheza England

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Dar24

Klabu za Arsenal na Liverpool kutoka England zimeripotiwa kuwa na mpango wa kuiwania saini ya Kiungo wa Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich, Joshua Kimmich ambaye mustakabali wake katika timu yake ya sasa unazidi kuwa shakani.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 29, anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao, huku Sky Germany ikiripoti kuwa, mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yamesimama.

Kusuasua kwa mazungumzo ya kuongezwa mkataba mpya kumemfanya nyota huyo kufikiria mchakato wa kutaka kutimkia timu nyingine katika dirisha kubwa la usajili, huku Bayern ikilazimika kumuuza ili kutomuacha bure pale mkataba wake utakapomalizika.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Ujerumani, Arsenal ni miongoni mwa klabu zinazovutiwa na saini ya nyota huyo anayewaniwa na klabu za Manchester City, Liverpool, Real Madrid na FC Barcelona.

Mkongwe huyo aliyecheza mechi 82 katika timu ya taifa ya Ujerumani, ameshinda mataji 20 tangu alivyojiunga na Bayern Munich akitokea RB Leipzig katika majira ya kiangazi mwaka 2015.

Mchezaji huyo amefunga bao moja na kutoa pasi tano za mabao katika michezo 20 za Ligi Kuu ya Ujerumani msimu huu, huku Bayern Munich ikishika nafasi ya pili kwa alama 60 baada yya kushuka dimbani mara 26.

Kinara Bayern Leverkusen imevuna alama 70 katika michezo 26 hadi sasa msimu huu, ikishinda mechi 22 na kutoka sare katika michezo minne.

Chanzo: Dar24