Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joseph Guede: Wananchi mtafurahi

Joseph Guede Ds Joseph Guede.

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Joseph Geude raia wa lvory Coast hatimaye amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na timu hiyo kupitia dirisha dogo lililofungwa Jumanne ya wiki hii.

Mshambuliaji huyo amekuja kuchukuwa nafasi ya mshambuliaji Hafiz Konkoni ambaye ametolewa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Dogan Birligi ya nchini Cyprus.

Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Ivory Coast, mshambuliaji huyo amesema kuwa anakuja Tanzania rasmi kuanza kazi ya kuipambania Young Africans, huku akiamini kuwa atafanya vyema pia akiweka wazi shauku yake ya kuanza kukipiga ndani ya timu hiyo.

“Wananchi muda si mrefu nakuja Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nawapa furaha, nafurahi kujiunga pamoja nanyi kwenye hii timu, naamini kuwa kila kitu kitakuwa sawa hapa na tutafurahi pamoja,” amesema mshambuliaji huyo.

Young Africans kupitia dirisha dogo la usajili imefanya usajili wa wachezaji wawili tu wa kimataifa ambao ni winga Mghana Augustine Okrah na mshambuliaji Joseph Guede, huku kwa wazawa akiwa ni Shekhan Hamisi pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: