Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joseph Guede; Huu si wakati wa kusikilizia kivuli cha Mayele

Joseph Guede Yanga Joseph Guédé Gnadou

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati jumba la ma onyeshe likiwa limebeba picha mbali mbali za Fiston Kalala Mayele, ni jina la Kennedy Musonda lilikuwa likiwekwa kando za frame za mfalme yule aliyetoweka na kutimkia kwa Mafarao wa Misri.

Ni kivuli cha Mkongomani Fiston Mayele kilitufanya tuamini miguu ya Kennedy Musonda isingeweza kuthubutu kuvaa viatu vya mfalme yule, bado tumeendelea kuamini hivyo mpaka leo.

Wakati mabaki ya kumbukumbu ya Fiston Mayele yakiendelea kutafuna mioyo ya mashabiki wa Yanga, Hafiz Konkoni aliibuka chambo kwenye kurejesha furaha. Wananchi walikopesha imani ambayo waliamini ingerudi na riba, lakini Konkoni hakuweza kulipa imani ile.

Joseph Guede anakuja wakati mioyo ya mashabiki wa Yanga imeshafubaa kwa mateso ya kukosa imani dhidi Mzize, Musonda na Konkoni. Mbaya zaidi Watanzania hatujawahi kusujudu neno 'ngoja tumpe muda'. Si kwa Simba wala Yanga, mashabiki wanaweza kukuhukumu kwa dakika ishirini tu ulizocheza.

Kwa Joseph Guede kwake si wakati wa kusikiliza kivuli cha Filton Mayele. Ni ukweli usiofichika inabidi kwanza ajiweke fit kuanzia akili hadi mwili ili awe bora kuliko jana.

Wakati huu imani ya wananchi iliyozaliwa kwenye mifumo yao ya ufahamu inaweza kuwalipa na fidia. Uchezaji wake, nguvu, stamina, ataweza kumudu vyema ligi letu. Wananchi waamini kwenye muda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live