Kocha Mkuu wa AS Roma, Jose Mourinho anaamini Inter Milan ni timu ya kiwango cha juu sana msimu huu 2023/24, huku Juventus ikiimarika zaidi chini ya Kocha Massimiliano Allegri.
Kocha huyo wa kimataifa wa Ureno alizungumza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi dhidi ya SS Lazio, kama ilivyoripotiwa na FCInterNews.
Ila amekosolewa bado ni mapema kusenma mbio za ubingwa wa Serie A itakuwa kati ya Inter Milan na Juventus.
Lakini mechi za mwishoni mwa juma lililopita AC Milan, SSC Napoli, Atalanta, SS Lazio na AS Roma zote zilipoteza pointi muhimu, wakati Inter Milan na Juventus zikiibuka na ushindi.
Hii ina maana timu hizo mbili zilizo kileleni zina uongozi kwa pointi nyingi tofauti na timu nyingine msimu huu 2023/24.
Wakati huo huo, uwiano wa pointi kati ya Inter na Juventus ni ndogo kwenye msimamo. Inter (pointi 29) imezidivwa pointi mbili dhidi ya wapinzani wao wa Juventus (pointi 31).
Lakini ukweli ni timu hizo mbili zitamenyana baada ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa na utakuwa mchezo wa upinzani mkali kutokana na ubora wao msimu huu 2023/24.
Mourinho alisema Tumerudi na pointi tatu [kutoka nne bora] kwa sababu ya jinsi msimu ulivyokwenda. Kuna Inter, ambao ni timu nzuri.” alisema.
“Kisha Juventus, ambao ni timu nzuri na kocha mzuri pia. Lakini kuna timu kama SSC Napoli ambayo ilifungwa dhidi ya Empoli, au Milan iliyochezea kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Lecce,” Mourinho alitania. “Yaani namaanisha, samahani zilitoka sare ya mabao 2-2.”
Kocha wa Inter, Inzaghi anasaka ubingwa wa Serie A kwa mara ya kwanza lakini aliwahi kushinda mataji ya kwenye mashindano kama Coppa Italia na alitinga fainali ya Ligi Mabingwa Ulaya msimu uliyopita dhidi ya Manchester City.