Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jorginho aweka rekodi ya kibabe EPL

JORG Kiungo wa Chelsea, Jorginho aweka rekodi EPL

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: eatv.tv

Kiungo wa chelsea Jorginho Frello ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi kuu ya Uingereza, kufunga Penati kumi ndani ya mwaka mmoja baada ya kuweka kimyani mikwaju miwili dhidi ya Aston Villa katika ushindi wa 3-1.

Kwenye mashindano yote Jorginho ashikilia rekodi ya kufunga penati 23 kati ya 26 tangu atue ndani ya the Blues mwaka 2018 akiwa na jumla ya magoli 25, katika michezo 118.

Rekodi hii inaweza kuongeza siku ya Jumatano katika mechi ya mwisho ambayo Chelsea watacheza dhidi ya Brighton & Hove Albion katika dimba la Stamford Bridge kwenye mchezo wa mwisho wa mwaka wa EPL.

Jorgihno anamaliza mwaka kwa mafanikio makubwa baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwenye Bara la ulaya, baada ya kushinda mataji matatu muhimu ambayo ni UEFA Champions League, UEFA Super cup, pamoja na UEFA Euro akiwa na timu ya taifa ya Italy.

Chanzo: eatv.tv