Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jopo la madaktari Yanga lamruhusu Aucho kuwavaa Dodoma Jiji leo

Aucho Job Sta Khalid Aucho na Dickson Job

Wed, 10 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jopo la Madaktari wa Yanga, limethibitisha kuwa kiungo wao mkabaji Mganda, Khalid Aucho yupo fiti na tayari kuwavaa Dodoma Jiji leo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Tanzaniaweb.com, kiungo huyo amepata utimamu mwili kwa sasa na kesho yupo fiti kuwavaa Dodoma.

Kiungo huyo tangu amerejea nchini akitokea Afrika Kusini wakati timu hiyo, ilipokwenda kucheza mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, kiungo huyo ameonekana kufanya mazoezi magumu, hivyo kilichobakia ni maamuzi ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi kumtumia au asimtumie kesho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live