Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jokate amwanika mwanaye, wadau wampongeza

Jokate Mentioned Jokate amwanika mwanaye, wadau wampongeza

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amejitokeza hadharani na kuachia picha ya mwanaye ikiwa zimepita wiki kadhaa tangu alipojifungua.

Licha ya kutomuonesha sura ya mwanaye huyo kwa wafuasi wake kwenye mtandao wa Twitter, leo tarehe 28 Disemba, 2022 Jokate alibandika picha inayomuonesha amembeba mwanaye huyo na kusindikiza na ujumbe wa kumshukuru Mungu.

Katika andiko hilo Jokate aliandika ‘Mama totoo, Glory to God’. Ujumbe huo pamoja na picha zilipokewa vema na wafuasi wake mkuu huyo wa wilaya ambaye amejizolea umaarufu tangu alipoanza kutumikia nafasi hiyo ya kisiasa.

Mkurugenzi mtendaji wa Simba, Barbara Gonzalez alikuwa wa kwanza kumpongeza Joketi kwa kuandika; ‘Congratulatio my dear Jojo aka Mama toto.”

Naye mwanadada maarufu ambaye pia ni dada yake Waziri wa Nishati, Januari Makamba, Mwamvita Makamba alimpongeza Jokate kwa kufanikiwa kupata mtoto.

Licha ya kwamba hadi sasa Joketi hajamwanika baba wa mtoto, huku mfanyabiashara Fred Vunjabei akitajwa tajwa na wadau kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live