Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Johora fresh tu Jangwani

Erick Johora Mlinda mlango wa Yanga, Erick Johora

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nyie subirini tu muone! Ndicho alichosema kipa wa Yanga, Erick Johora ambaye alipata nafasi kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2022/23, kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi FC.

Johora ambaye ni chaguo la tatu kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi, alisema amekuwa akipambana mazoezini ili kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha timu hiyo kama ilivyo kwa Djigui Diarra na Abutwalib Mshery.

“Kufanya kazi kwa bidii mazoezini ndio kitu pekee ambacho nilikuwa nikiweka juhudi kwa sababu niliamini kuna siku nitapata nafasi, naamini kuwa huu ni mwanzo wa kuendelea kupata nafasi zaidi ya kucheza,” alisema.

“Nimekuwa na uhusiano mzuri na makipa wenzangu. Tumekuwa tukifanya kazi kwa ushirikiano, sote tupo hapa kwa ajili ya Yanga na hilo ndilo jambo muhimu kwetu kuliko masuala binafsi, mchango wa kila mchezaji ni muhimu kwenye timu.”

Tangu msimu huu wa Ligi kuu Bara uanze kipa huyu hajacheza mechi hata moja.

Chanzo: Mwanaspoti