Chelsea imethibitisha kwamba lejendi wao John Terry amerejea tena kwenye timu yao lakini safari hii atafanya kazi kama mshauri wa soka la vijana.
Terry, 41, atakuwa anarudi kwenye timu hiyo baada ya kuondoka miaka minne iliyopita ambapo alitimkia Aston Villa alipokuwa anafanya kazi kama kocha msaidi chini ya Dean Smith.
Katika taarifa iliyotolewa na timu hiyo ilieleza kuwa: 'Lejendi wa Chelsea atakuwa anafanya kazi na wachezaji wetu vijana na makocha katika mpango wetu wa maendeleo ya soka la vijana, atatupa kile alichokipata katika miaka 20 ya uchezaji wake sambamba na kufundisha kama kocha msaidizi.
Taarifa hiyo iliongeza kwamba Terry ataanza kazi mwezi ujao na majukumu yake ya ziada itakuwa ni kushauri makocha wa timu hizo za vijana na kuognoza wachezaji.