Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

John Terry Ajiandaa Kurudi Chelsea

Jt Nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki kisiki wa zamani wa klabu ya Chelsea John Terry anajiandaa kurudi tena kwenye klabu yake ya zamani baada ya miaka mitano kuchukua mikoba ya kuwa kocha wa timu ya vijana.

John Terry mwenye miaka 41 aliachana na klabu ya Chelsea na kutumia muda huo kufanya kazi za ukufunzi huku akitumia muda wa miaka mitatu kwenye klabu ya Aston Villa akiwa kama kocha msaidizi wa Dean Smith kabla ya kuondoka majira ya kiangazi.

Kapteni huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuachana na klabu ya Aston Villa alizunguka nchi mbalimbali za Ulaya akijifunza aina tofauti ya mifumo ya ukocha na kusubiri kazi mpya ya ukufunzi itakayopatikana.

Baada ya kuona wachezaji wenzie wa zamani kama Wayne Rooney, Frank Lampard na Steven Gerrard wakianza kufanya kazi zao kwa mara ya kwanza nje ya ligi kuu ya Uingereza, Terry nae anaamini anaweza kupitia njia hiyo pia.

Kwa sasa John Terry anaishi karibu na uwanja wa mazoezi wa Cobham na ameripotiwa kuwa na ukaribu na wachezaji wenzie wa zamani Petr Cech and Carlo ambao wamepata kuajiriwa na klabu ya Chelsea pia inesemekana mkurugenzi wa akedemi Neil Bath anamsaidia ili aweze kurejea tena kwenye klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live