Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula amesema klabu hiyo imemtoa mshambuliaji wake John Bocco kutoka kuwa nahodha wa timu hiyo na sasa anafundisha timu ya vijana ya Simba.
Kajula ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi, Mei 16, 2024 ambapo baadaye klabu hiyo itazindua Simba Executive Network yenye lengo la kuimarisha uongozi wa klabu hiyo.
Kajula amesema klabu ya Simba ina viongozi wanaoamini katika muendelezo wa wachezaji na watu mbalimbali, aidha Kajula amesema kuwa klabu hiyo itafanya mabadiliko muhimu ambayo yataendana na ripoti ya wataalamu na maeneo ambayo bodi itaona ni muhimu kwa kufuata utawala wa sheria.