Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

John Bocco aongezwa Taifa Stars kuwamaliza Uganda

Bocco John Rafael.jpeg John Bocco

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mkongwe wa Simba SC, John Raphael Bocco ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kuelekea mchezo wa marudiano na Uganda kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Jumamosi Uwanja wa St. Mary's Kitende mjini Entebbe.

Uteuzi huo umefanywa na makocha wapya wa muda, Mzambia Hanoor Janza na Msaidizi wake, Mecky Mexime na kocha wa makipa, Juma Kaseja siku mbili tu tangu wapewe jukumu hilo.

Ikumbukwe juzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimuondoa kazini kocha Mdenmark, Kim Poulsen na wasaidizi wake kufuatia Taifa Stars kuchapwa 1-0 na Uganda katika mechi ya kwanza ya hatua hiyo ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya CHAN Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa jumla atafuzu Fainali za CHAN ambazo zitafanyika nchini Algeria kuanzia Januari 8 hadi 31.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live