ARSENAL imetuma barua kwenda PSV Eindhoven kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa timu hiyo na Ubelgiji, Johan Bakayoko, 21, dirisha hili.
Kwa sasa Bakayoko pia anahitajika Liverpool na Bayern Munich lakini Arsenal ndiyo inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumpata kutokana na pale walipofikia.
Timu nyingi zimeonyesha nia ya kumsajili staa huyu kutokana na kiwango bora alichoonyesha msimu uliopita na alifunga mabao 12 na kutoa asisti tisa katika mechi 33 za Ligi Kuu Uholanzi.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, saini yake inaweza kupatikana kwa kiasi kisichozidi Pauni 40 milioni.
Hata hivyo, hakuna timu iliyofikia mwafaka wa moja kwa moja kumsajili na inawezekana Arsenal ikapinduliwa katika dili hilo kama itazubaa.
Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.
Alipita timu za vijana za OH Leuven, Club Brugge, Mechelen na Anderlecht, kabla ya kujiunga PSV Eindhoven mwaka 2019.
CHELSEA ipo katika hatua za mwisho kulipa Euro 6 milioni kwenda Barcelona ili kuipata saini ya straika wa timu hiyo na Hispania Marc Guiu, 18, katika dirisha hili. Mabosi wa Chelsea wamevutiwa sana na kiwango cha staa huyu alichoonyesha msimu uliopita. Mkataba wa Marc unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao tisa.
WEST Ham imepanga kumuuza mshambuliaji wake raia wa England, Danny Ings, 31, katika dirisha hili la uhamisho la majira ya kiangazi na Southampton ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kuipata huduma yake.
Taarifa zinaeleza, West Ham inataka kuachana na staa huyu wa zamani wa Liverpool kwa sababu hayupo katika mipango ya benchi la ufundi kwa msimu ujao.
KOCHA wa Manchester United, Erik ten Hag amewaambia viongozi wa timu hiyo anahitaji kiungo wa kati katika dirisha hili na moja ya majina aliyoyawasilisha ni la kiungo wa PSG, Manuel Ugarte, ambaye ndio chaguo lake la kwanza. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa, Man United imeshaanza hadi mazungumzo kwa ajili ya kukamilisha usajili wa fundi huyu raia wa Uruguay.
MANCHESTER United huenda ikabadili gia angani na kuanza mazungumzo na Everton kwa ajili ya kumsajili straika wa timu hiyo Dominic Calvert-Lewin katika dirisha hili ikiwa itaikosa saini ya straika wa Bologna na Uholanzi, Joshua Zirkzee, 23. Mkataba wa sasa wa Lewin unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Msimu uliopita alicheza mechi 38 za na kufunga mabao manane.
NOTTINGHAM Forest ipo hatua za mwisho kwa ajili ya kumsajili straika wa timu hiyo na Jamaica, Michail Antonio, katika dirisha hili.
Antonio mwenye umri wa miaka 34, ikiwa atajiunga na Nottingham itakuwa ni mara ya pili baada ya kuichezea hapo awali kuanzia mwaka 2014 hadi 2015. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa wiki hii.
AC Milan imemweka katika rada zao beki wa Barcelona, Inigo Martinez katika dirisha hili, inaripoti Mundo Deportivo.
Staa huyu wa zamani wa Athletic Bilbao, anataka kuondoka Barca kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha wababe hao kutoka viunga vya Nou Camp. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.
Juventus inahitaji kati ya Pauni 27 na 35 milioni ili kumuuza.
BEKI wa kati wa Real Madrid, Nacho anatarajiwa kuondoka rasmi katika timu hiyo mwisho wa wiki hii na mkataba wake unatarajiwa kumalizika na anahusishwa katika mpango wa kujiunga na mojawapo ya timu huko Saudi Arabia. Staa huyu raia wa Hispania msimu uliopita alicheza mechi 46 za michuano yote na kutoa asisti moja.
Licha ya mazungumzo hayo kwenda vizuri hadi sasa bado hakuna muafaka wowote uliofikiwa baina ya pande zote mbili kuhusiana na ada ya uhamisho.