Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joe Gomez kuipiga kibuti Liverpool

Joe Gomez Liver.jpeg Joe Gomez

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Liverpool, Joe Gomez ameripotiwa kuwa na mpango wa kwenda kukabiliana na changamoto mpya baada ya Newcastle United kuonyesha dhamira ya dhati ya kunasa saini yake.

Gomez, 27, amekuwa mchezaji muhimu kwa kipindi cha miaka tisa wakati Jurgen Klopp alipokuwa akiinoa miamba hiyo ya Anfield, lakini sasa Mjerumani huyo ameondoka na kumfanya beki naye kufikiria kuondoka.

Gomez alicheza mechi 32 kwenye Ligi Kuu England katika kikosi cha Liverpool msimu uliopita, ambapo alianza kwenye mechi 17 na kuasisti mara moja akitamba kwenye nafasi hiyo ya beki.

Kutokana na kumudu kucheza namba nyingi uwanjani, beki huyo alipata nafasi ya kujumuishwa kwenye kikosi cha England chini ya kocha Gareth Southgate kilichokwenda kwenye fainali za Euro 2024 huko Ujerumani.

John Stones, Marc Guehi na Ezri Konsa walipata nafasi ya kuanza mbele ya Gomez kwenye beki ya kati, ambapo staa huyo wa Liverpool alitumika kwenye mechi za kirafiki tu dhidi ya Bosnia Herzegovina na Iceland.

Ripoti zinafichua kwamba Gomez anataka kuzihitimisha nyakati zake bora kwenye kikosi cha Liverpool kwa kuachana na timu hiyo kabla ya dirisha hili la usajili wa majira ya kiangazi huko Ulaya kufungwa.

Msimu ujao, Liverpool itakuwa chini ya kocha mpya Mdachi, Arne Slot, aliyetua kutoka Feyenoord na inatazamwa kama Gomez atakuwa kwenye mipango ya kocha huyo kuendelea kupiga kazi Anfield.

Chanzo: Mwanaspoti