Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job awatega mastraika Yanga

Aziz Maxi Job WA0019 Job awatega mastraika Yanga

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga tayari ipo mjini Kumasi kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Medeama, huku beki na nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job amewatega mastraika kwa kuwataka kutumia nafasi watakazopata kufunga mabao wakati mabeki wakijilinda, ili timu itoke na ushindi wa kwanza katika Kundi D wa Ligi ya Mabingwa.

Yanga inakutana na Medeama katika mechi ya raundi ya tatu ya kundi hilo, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Baba Yara jijini Kumasi, Ghana, ikiwa imevuna pointi moja tu iliyopata mbele ya watetezi, Al Ahly ya Misri baada ya awali kufungwa mabao 3-0 na CR Belouizdad zinazovaana leo.

Akizungumza Job alisema wanatambua kwamba wanakwenda kucheza mchezo mwingine mgumu ugenini lakini akasema kama washambuliaji wao watafanya kweli kwa kutengeneza nafasi na kuzitumia mechi itakuwa rahisi kwao.

Job alisema wao kama mabeki wamefuatilia ubora wa safu ya ushambuliaji ya wapinzani wao kisha wakajipanga sawasawa kuhakikisha wanaongeza umakini kuhakikisha hawaruhusu mabao ugenini.

“Hii ni mechi ngumu lakini sisi Yanga tuna ubora wetu sio kitu kipya kwetu kuweza kushinda ugenini hata hii mechi mimi tunatakiwa kufunga mabao ya kutosha,” alisema Job na kuongeza;

“Mabeki tumejipanga sawasawa hatutaki kuyarudia makosa ya nyuma timu nzima ilicheza vizuri mechi iliyopita tunataka umakini ule uongezeke.”

Pia, Job aliongeza wanitambua alama tatu za mechi hiyo zitawarudisha kwenye utulivu wa kupigania malengo yao ya kuweza kutinga hatua ya robo fainali.

“Hii mechi kama tukishinda itatusaidia kufufua malengo yetu ya kucheza robo fainali, tunayataka matokeo kuliko wapinzani wetu kwa sasa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: