Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job afunguka siri waliyopewa na Gamondi vyumbani kuwamaliza Waarabu

Dickson Job Yanga Xd Job afunguka siri waliyopewa na Gamondi vyumbani kuwamaliza Waarabu

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Klabu ya Soka ya Yanga, Dickson Job amesema kuwa walijiandaa vizuri ndiyo maana walifanikiwa kuwafunga CR Belouizdad mabao 4-0 na kutinga robo fainali ya CAFCL kwa kishindo.

Gamondi alisema hayo akiwa na furaha baada ya kuandika rekodi nyingine akiiongoza timu yake kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Belouizdad licha ya kufungwa bao 3-0 katika mchezo wa kwanza kule Algeria.

“Maandalizi yalikuwa mazuri sana na tulitegemea hiki ambacho tumekipata na kama tungekuwa makini tungewapiga zaidi ya bao 4. Belouizdad wana timu bora lakini sisi tulijiandaa vizuri zaidi ndiyo maana tukapata matokeo.

“Walikuja kujilinda kipindi cha kwanza ili kipindi cha pili watushambulie kwa kushitukiza, mwalimu aliliona hilo tuliporudi kwenye vyumba akatuambia bao moja halitoshi inabidi tuongeze, ndiyo maana tuliingia kipindi cha pili kwa kuwa-press kwa nguvu tukafanikiwa kupata mabao manne.

“Mashabiki zetu Wananchi wamefanya balaa, muda wote tangu mechi inaanza mpaka inamalizka walikuwa wanaamsha amsha tu, hongereni sana mashabiki zetu,” amesema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: