Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job aanika siri nzito Yanga SC

Papy Pic Data Job aanika siri nzito Yanga SC

Sun, 7 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

YANGA ndio klabu ya pili iliyoruhusu mabao machache ikiwa nyuma ya Simba ambayo haijafungwa bao lolote hadi sasa, lakini siri inayoibeba ngome ya vijana hao wa Jangwani imefichuliwa na beki Dickson Job, aliyedai kuwepo kwa viungo bora na wazoefu imechangia kuwafanya wawe imara zaidi.

Job anayesimaama sambamba na nahodha wake, Bakari Mwamnyeto alisema viungo wao wakabaji walio bora wamewafanya wasiwe na kazi kubwa ya kulilinda lango lao na kumsaidia kipa wao, Diarra Djigui aliyeruhusu bao moja tu hadi sasa wakati wakiifumua Ruvu Shooting kwa mabao 3-1.

Akizungumza na Mwanaspoti, Job alisema wamekuwa imara sana eneo la beki baada ya ingizo la Khalid Aucho na Yannick Bangala na kuweka wazi kuwa wawili hao wameongeza utulivu na umakini kwenye eneo lao.

“Tunacheza na walimu kiwanjani ukiachana na kocha Nabi tumeongezwa nguvu kubwa ambayo imekuwa na msaada kwetu, hatufanyi makosa ya kizembe,” anasema na kuongeza;

“Aucho na Bangala ni wazoefu na wamecheza mashindano mengi makubwa, wamekuwa wakitoa maelekezo uwanjani, kitu ambacho kimetuongezea umakini na kutufanya kuwa bora, huwezi kutoa pasi ya ovyo na ndefu kutokana na wawili hao kukaa maeneo sahihi na ndio wanaotumika kutengeneza mashambulizi.”

Job alisema mwanzo zilikuwa zinatumika sana pasi ndefu kutafuta mawinga ambao ndio walikuwa wanatengeneza mashambulizi lakini kwasasa Yanga inaweza kutengeneza mashambulizi kuanzia kwa kipa Diarra.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz