Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job aahidi raha Yanga

7744fb671be6c3b2daa59550705d21d8 Job aahidi raha Yanga

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BEKI mpya wa Yanga, Dickson Job ameanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuahidi kuwapa raha mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo.

Job aliyesajiliwa katika dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar alisema Dar es Salaam jana kuwa ana amini yupo sehemu sahihi na kuahidi kujituma na kushirikiana na wenzake kusaidia timu kuchukua taji la ligi.

“Hapa nipo sehemu ya furaha kwani ni historia katika maisha yangu, sababu nilikuwa naota kuja kucheza timu kubwa mojawapo Tanzania,” alisema.

Alisema anashukuru amepokelewa vizuri na kupata ushirikiano na kazi yake kubwa ni kujituma uwanjani pale atakapopata nafasi.

“Mtarajie makubwa sababu mmeniamini nahitaji kuthibitisha kile nilichokuwa ninakionesha nikiwa Mtibwa.” Alisema.

Job ni kati ya wachezaji watatu waliosajiliwa na Yanga kwenye dirisha dogo, wengine ni Saido Ntibazonkiza na Fiston Abdoul Razack.

Katika hatua nyingine, Msemaji wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema wachezaji wa timu hiyo wameingia kambini kujiandaa na mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema wachezaji wote wapo vizuri na malengo yao ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zijazo za mzunguko huo na kuchukua taji.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze alisema wanajipanga kwa ajili ya michezo ijayo na muhimu ni kuendeleza kasi waliyoanza nayo.

Alisema mechi za mzunguko wa pili ana amini zitakuwa na ushindani mkubwa hivyo ni lazima wajipange vizuri.

Kaze alisema wachezaji waliokuwa majeruhi Saido na Yacouba Songne huenda wakajiunga na wenzao kuanzia leo.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanzia Februari 13, huku Yanga ikitarajiwa kuanzia dhidi ya Mbeya City na baadaye kurudi Dar es Salaam kuisubiri Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.

Chanzo: habarileo.co.tz