Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Vilabu vinawachonganisha wachezaji na mashabiki

Kibu Kuwasili.jpeg Kibu Denis

Sat, 4 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

George Job, Mchambuzi wa Soka wa kituo cha Wasafi FM anafunguka kuhusu tabia za vilabu vya Bongo kuwaacha wao bila makubaliano yoyote wakati mikataba yao inapoelekea mwishoni kisha kuja kuwashitukiza wakiwa na wao wameshafanya maamuzi mengine.

Kauli hii ya Job inakuja ikiwa taarifa zimesambaa kuwa Kibu Denis ameigomea Simba kusaini kandarasi mpya akitaka mtonyo mrefu.

"Vilabu vyetu ni mabingwa wa kuset ajenda... wanaweza kumuacha mchezaji mpaka miezi michache ya mwisho ya mkataba wake kisha wakaibuka dakika za mwisho, na hapo hawataki kusikia jibu la hapana kutoka kwa mchezaji. Unapo muacha mchezaji mpaka dakika za jioni unataka afanyaje?

"Mchezaji unapomuacha mpaka miezi ya mwisho ni haki yake kuanza kuangalia mustakabali wa maisha yake mapya, mchezaji yoyote mwenye akili hizi ndio hatua anazo chukua. Lakini mara nyingi inapo fikia hapa, vilabu hutumia njia ya kuwachonganisha wachezaji na mashabiki.

"Utasikia tu "tulimpa ofa akakataa". Sawa mmempa ofa lakini ni wakati gani? Kama mmempa ofa wakati ambao tayar kafanya maamuzi mengine mnataka asemaje? Siku tukisikia upande wa wachezaji tutashika vichwa," George Job, Mchambuzi wa Soka wa kituo cha Wasafi FM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live