Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Tupo tayari kuwakabili Ihefu

Yanga Dom 004 Job: Tupo tayari kuwakabili Ihefu

Sun, 19 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha msaidizi na beki wa kati wa Young Africans SC, Dickson Job amesema kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Ihefu, wao kama wachezaji wapo tayari kuwapa furaha Wananchi.

Leo Jumapili, Young Africans watacheza mechi ya nusu fainali ya CRD Federation Cup dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kuanzia saa 9:30 alasiri.

“Kwa upande wetu sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri, nadhani upande wa benchi la ufundi wameshamaliza maelekezo yao, kwa hiyo tunachoomba kesho (leo) kuamka salama na kuweza kuipambania nembo ya Yanga na kupata matokeo katika mchezo huo.

“Napenda kuwaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo, sisi wachezaji tuko vizuri na tumejipanga vizuri kuwapa furaha katika mchezo huo.

“Kwa sasa tunaangalia kwanza mchezo wa kesho tuweze kufanya vizuri ili kulitetea kombe letu tulilochukua msimu uliopita. Wajitokeze kwa wingi na ninaamini kwa uwezo wa Mungu furaha itapatikana,” alisema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live