Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Tunazitaka alama 3 za Mashujaa

Jobbb A0010 Job: Tunazitaka alama 3 za Mashujaa

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha Msaidizi wa kikosi cha Yanga, Dickson Job, amesema maandalizi ya kwenda kuifunga Mashujaa yamefanyika ambapo kila mchezaji anatambua lengo kuu ni kwenda Kigoma kuchukua pointi tatu.

Job ametoa kauli hiyo wakati leo Jumapili kikosi hicho kitakuwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma kucheza dhidi ya Mashujaa katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Job amesema: “Kikubwa tunafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mashujaa kwa hiyo sisi kama wachezaji tuko tayari kwa ajili ya kupamabana, tutaenda kupambana kwa asilimia mia ili kupata matokeo mazuri ili kuendelea kujihakikishia nafasi tuliyopo.

“Naamini mchezo utakuwa mgumu kwa sababu Mashujaa nayo ni timu nzuri lakini pia katika nafasi waliyopo wanazihitaji pointi tatu, sisi pia tunahizitaji hizo pointi kwa sababu ni moja kati ya pointi zinazokwenda kutupa ubingwa.

“Morali ipo vizuri, kila mchezaji yupo vizuri na anahitaji kuitumikia timu ili mwisho wa siku sote kwa pamoja tuweze kuchukua ubingwa.

“Ningependa kuwaomba Wanakigoma mjitokeze kwa wingi lakini pia mikoa ya jirani tunawaomba mjitokeze kwa wingi katika mchezo huo dhidi ya Mashujaa na sisi vijana wetu tutapambana kwa asilimia mia kuweza kuwapa furaha.

“Lakini hata wale waliopo Dar es Salaam dua zao ni muhimu, unapokuwa unaangalia mpira kwenye TV tunahitaji dua zako ili tupate matokeo mazuri kwenye mchezo huu.”

Young Africans itaingia uwanjani kwenye mchezo huo ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha pointi 62, huku zikihitajika pointi 11 pekee katika michezo sita iliyobaki ili kutetea ubingwa wetu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live