Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Tunawajua Mamelodi, hatutacheza kwa kuwaogopa

Job: Tunawajua Mamelodi, Hatutacheza Kwa Kuwaogopa.jpeg Job: Tunawajua Mamelodi, hatutacheza kwa kuwaogopa

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Yanga, Dickson Job amesema wanaifahamu vizuri Mamelodi Sundowns na wapo tayari kwa ajili ya kuvaana nao Jumamosi ijayo. Job ambaye ni nahodha msaidizi wa timu hiyo amesema wanafahamu ubora wa Mamelodi, lakini kwao wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanakabiliana nao ndani ya uwanja.

“Mazoezi tunayofanya yatakwenda kutoa picha halisi tutawezaje kushinda na kuwazuia wapinzani wetu, kwa kutumia ubora wetu na kikosi kipana tulichonacho, tumevuka hatua ngumu nyingi na kushinda sehemu ambayo wengi hawakutupa nafasi.

“Jambo zuri tuna kocha anayeijua Mamelodi na ni lazima atatupa mbinu ya kuwamaliza kwani anawafahamu vizuri, kwa kweli hatutacheza kwa hofu ya kuangalia jina la mchezaji au nchi kwani tunachotafuta ni ushindi utakaotupa wepesi wa kutinga nusu fainali, tunaamini tuna uwezo mkubwa wa kushinda mechi hii,” alisema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live