Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Tumejiandaa kuwakabili Ihefu

Job Goal Vs Sirri Job: Tumejiandaa kuwakabili Ihefu

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha Msaidizi Yanga SC, Dickson Job amesema kikosi chao kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho Oktoba 4, 2023 wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ihefu Fc ya mkoani Mbeya.

Job amesema mchezo utakuwa mgumu lakini kama wachezaji wamejipanga kufanya vizuri ili kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi kuu bila kutazama kuwa Ihefu ndiyo timu iliyoivunja unbeaten ya mechi 49 ya Yanga msimu uliopita.

"Sisi kama wachezaji tumejiandaa kwa ajili ya kupambana na kuhakikisha tunapata alama tatu. Tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Ihefu ni timu nzuri, lakini lengo letu sisi ni ushindi tu.

"Baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, morali ya wachezaji wote iko juu na kila mmoja anataka apambane ili kuipa ushindi timu yake, kwa hiyo utakuwa mchezo mzuri," amesema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: