Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Nitafunga tena

DICKSON JOB KAZINI Dickson Job

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa kati wa Yanga, Dickson Job amesema kutokana na historia aliyoiacha kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro anaamini mchezo dhidi ya KMC utakaopigwa keshokutwa atafunga tena.

Mechi ya kwanza msimu huu ambapo Yanga ilicheza na KMC katika Ligi Kuu Bara, Job alifunga bao moja katika dakika ya 17 kwenye ushindi wa mabao 5-0 ilioupata timu hiyo katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi Agosti 23, mwaka jana.

Lakini, Job amesema ishu ya ukimya kwake siyo jambo kubwa na kwamba kwa kuwa anaufahamu vyema Uwanja wa jamhuri ambao ndio umekuza kipaji chake, basi watu wasubiri atafunga bao.

"Nina historia nyingi katika makuzi yangu ya mpira mazuri na mabaya na nakumbuka niliwahi kufunga penalti hivyo naamini mechi na KMC nitafunga," amesema mchezaji huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea Mtibwa Sugar.

Yanga iko katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi na pointi 40, Simba 33, Azam FC nafasi ya tatu na pointi 32.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: