Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Job: Augsburg ni kipimo sahihi kwetu

Yanga Augsburg Job: Augsburg ni kipimo sahihi kwetu

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha Msaidizi wa Young Africans SC, Dickson Job amesema mchezo waliocheza dhidi ya Augsburg ya Ujerumani ni kipimo sahihi kwa timu yao.

Juzi, Yanga walicheza mechi ya Mpumalanga Cup dhidi ya Augsburg inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani maarufu Bundesliga na kupoteza kwa magoli 2-1.

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mbombole uliopo Mji wa Mpumalanga nchini Afrika Kusini, Yanga walitengeneza nafasi 14 na kupiga mashuti matano yaliyolenga lango la wapinzani huku wakifunga goli moja kupitia Jean Baleke.

“Tumepata mchezo mzuri na tumeona wapi tumefikia kwani tangu tumeanza maandalizi kama tuna wiki, kwa hiyo hiki ni kipimo kizuri na sahihi kwetu kwa sababu tumekutana na timu yenye levo ya juu kabisa.

“Tumejipima na tumeona ni wapi tumefikia, tunarudi katika maandalizi ya siku mbili tatu kwa ajili ya mchezo ujao ambao tutacheza hapahapa tunaamini kuna sehemu tutakuwa tumefikia kuelekea mchezo unaokuja.

“Kikubwa ndani ya timu kuna ushindani wa nafasi kila mchezaji anapambana kuonesha kilicho bora ili aweze kuingia kikosi cha kwanza.

“Jambo hilo katika timu yoyote inayohitaji mafanikio ni kitu kizuri kwa sababu tuna wachezaji wenye ubora mzuri, sisi kama wachezaji tuna wakati mzuri wa kupambana kila mchezo wa kirafiki kumuonesha mwalimu kile tulichonacho.

“Katika mpira wa miguu hakuna kitu kigumu kama kutengeneza nafasi, kama tunacheza na timu kubwa halafu tunaweza kucheza na kutengeneza nafasi ni kitu kizuri naamini hata mwalimu pia anaona kile ambacho anakileta kwetu kinafika vizuri.

“Naamini tunapoenda kukutana na timu yenye uwezo kama wetu au wachini tunaweza kutengeneza nafasi nyingi zaidi na kutumia,” alisema Job.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live