Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joao Palhinha ruhsa kuondoka Fulham

Arsenal Na Chelsea Kwenye Mbio Kumsaka Nyota Wa Fulham Joao Palhinha Joao Palhinha

Tue, 11 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fulham inahitaji Pauni 60 milioni kutoka kwa timu yoyote inayohitaji kumsajili kiungo wa Joao Palhinha, 28, katika dirisha hili. Bayern Munich ni moja ya timu zinazomhitaji na ilidaiwa kuwasilisha ofa ya Pauni 30 milioni ambayo ilikataliwa.

Mbali na Bayern huduma ya staa huyu pia inahitajika na Barcelona na Manchester United. Miamba hiyo inajipanga kwa msimu ujao na inasaka nyota wapya.

MANCHESTER United na Tottenham zipo kwenye vita kali ya kuiwania saini ya winga wa Crystal Palace, Eberechi Eze, 25, katika dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa England, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 31 za michuano yote.

Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Mabosi wa Man United wametenga pesa ndefu kwa ajili ya kuimarisha kikosi msimu ujao.

Newcastle imeachana na mpango wao wa kutaka kumsajili kipa wa Valencia na Georgia, Giorgi Mamardashvili, 23, baada ya kuambiwa anauzwa kwa Euro 35 milioni. Mabosi wa Newcastle wanahitaji huduma ya kipa huyu lakini hawapo tayari kutoa zaidi ya Euro 30 milioni.

Mkataba wa Giorgi unamalizika mwaka 2027 na kuna kila dalili akaondoka klabuni hapo na kutua kwengine.

WEST Ham ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili beki wa Udinese Nehuen Perez, 23, katika dirisha hili na tayari imeshatuma wawakilishi wake kwenda Italia ili kufanikisha mchakato wa kumsajili.

Nehuen unatarajiwa kumalizika mwaka 2027. Msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kutoa asisti moja.

MATUMAINI ya Atletico Madrid kuipata saini ya straika wa Manchester City na Argentina, Julian Alvarez katika dirisha hili yanaonekana kufutika baada ya Alvarez mwenyewe kusema hana mpango wa kuondoka dirisha hili kwani bado anaamini ana nafasi ya kucheza na kupata mafanikio akiwa na matajiri hao wa Jiji la Manchester.

BAYERN Munich imeanza mazungumzo na Chelsea kumsajili beki wa kati wa timu hiyo Levi Colwill, 21, dirisha hili. Moja ya maeneo ambayo kocha mpya wa Bayern Vincent Kompany anaona yana upungufu ni lile la ulinzi.

Katika msimu uliomalizika alicheza mechi 32 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029 na una kipengele cha kinachowaruhusu Chelsea kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi.

BENCHI la ufundi la Atletico Madrid limependekeza tena jina la kiungo wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 28, ili asajiliwe katika dirisha hili.

Awali Atletico ilijaribu kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana kwa Pauni 15 milioni lakini ilishindikana, hivyo wanahitaji kurudia tena ili kufanikisha hilo. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025.

Chanzo: Mwanaspoti