Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Joao Felix mambo si mambo Atletico

Joao Felix Joao Felix

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kwa mujibu wa Diego Simeone, Joao Felix anahitaji kufanya jitihada za ziada kurejesha umuhimu wake kwenye kikosi cha Atletico Madrid.

Joao Felix alifanya vyema msimu uliopita, na pia amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, msimu huu. Lakini hivi karibuni amekuwa akicheza chini ya kiwango.

Staa huyu amejikuta akiwa benchi kwa muda mrefu zaidi, akiwa amekosa kucheza kabisa kwenye gemu nne za La Liga zilizopita licha ya kuwa na hali nzuri ya kumruhusu kucheza.

Nyota huyu ana miaka 22 , na anahitaji kufanya jambo ili kurejea kwenye mstari. Staa huyu alionesha ishara nzuri kwenye mechi iliyopita, Atletico waliyopoteza dhidi ya Real Madrid.

Simeone anasema kuwa Staa huyu anahitaji kurejea kile alichokifanya Bernabeu ili aweze kuiondoa benchi mara kwa mara ;

“Wakati wote huwa nakuwa muwazi kwa wote na kwa kile ambacho ni muhimu zaidi kwa timu, na Joao ni sehemu muhimu. Anapaswa kurudia kile alichokifanya Bernabeu kwa dakika 45 alizozipata.” amesema Simneone

Chanzo: www.tanzaniaweb.live